Aina 5 ya vyakula vinavyosaidia kupata mapacha

HomeElimu

Aina 5 ya vyakula vinavyosaidia kupata mapacha

Watu wengi wanapendelea kupata watoto mapacha, lakini baadhi ya mambo kama umri, historia ya familia na maradhi yanaweza kusababisha ukashindwa kufanikiwa ndoto yako hiyo.

Walakini, lishe yako inaweza kukusaidia kuweza kupata watoto mapacha endapo utaizingatia.

  1. Vyakula vyenye asidi ya folic

Inaaminika kuwa 40% ya wanawake wanaotumia asidi ya folic ya ziada wakati wa kujaribu kupata ujauzito wanaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuzaa mapacha. Walakini, inashauriwa kushauriana na daktari wako kwa kipimo kilichopendekezwa.

Vyakula vilivyo na asidi ya folic ni pamoja na parachichi, broccoli, kabichi, mchicha, kunde, avokado, ini, tambi na nafaka za kifungua kinywa.

  1. Mizizi ya maca

Kwa miaka mingi, mizizi ya Maca pia inajulikana kama Ginseng ya Peru imethibitishwa kuwa ya manufaa katika kuongeza uzazi. Tiba hii ya uzazi ambayo husaidia kusawazisha na kurekebisha homoni za wanawake inatajwa kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito wa mapacha. 

  1. Viazi Vikuu

Viazi vikuu ni chanzo kikubwa cha progesterone na phytoestrogens ambayo inaweza kusababisha kupevuka kwa mayai na hivyo kuongeza uwezekano wako wa kuzaa watoto wengi. 

  1. Maziwa

Mwanamke anapotumia kiasi kikubwa cha maziwa, huwa na uwezekano wa kutoa zaidi ya yai moja wakati mayai yakiwa yanapevuka na hii huongeza uwezekano wake wa kupata mapacha wasiofanana.

  1. Mihogo

Mihogo kama viazi vikuu, inajulikana kwa kuongeza rutuba. Pia husaidia kuongeza uwezekano wa kupata mapacha wajawazito.

 

error: Content is protected !!