Wakazi wa jiji la Mwanza waliojenga maeneo ya milimani wanatarajiwa kuondolewa ili kupisha wawekezaji kutoka nchini Brazil.
Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine, alisema mpango huo unalenga kuboresha miundombinu pamoja na kukuza sekta utalii utakaogharimu Sh bilioni 150.
Constantine alisema maeneo mengine ambayo wawekezaji hao wanayalenga ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha pembejeo za kilimo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Kanda ya Ziwa.
“Sehemu nyingine ni ujenzi wa barabara pamoja na nyumba za ghorofa katika milima mbalimbali ambayo inaangalia fukwe za Ziwa Victoria,” alisema Constantine.
Meya huyo alisema pia, Jiji limepewa jukumu la kulipa fidia katika maeneo ya Igogo, Isamilo na Kegoto ambayo yapo milimani ili kupisha uwekezaji huo.