Maombi ya wanachama 19 wa zamani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kibali cha kupinga kufukuzwa uanachama, yatajulikana leo Mahakama itakapotoa uamuzi wa pingamizi walilowekewa na chama hicho.
Halima Mdee, aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) na wenzake 18, wamefungua maombi, Mahakama Kuu Dar es Salaam, wakiomba kibali cha kupinga uamuzi wa chama hicho kuwavua uanachama.
Chadema kupitia jopo la mawakili wake linaloongozwa na Peter Kibatala wameweka pingamizi wakiiomba Mahakama hiyo isiyasikilize maombi hayo, wakidai kuwa yana kasoro za kisheria huku wakibainisha hoja sita.