Mwanaume akutwa na sehemu za siri 5 za mwanamke

HomeKitaifa

Mwanaume akutwa na sehemu za siri 5 za mwanamke

Mkazi wa Maswa mkoani Simiyu, Salum Nkonja maarufu kama Emmanuel Nkoja amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka 11, yakiwemo ya kukutwa na sehemu za siri za wanawake, chuchu na mafuvu mawili ya binadamu.

Miongoni mwa mashtaka hayo ni kukutwa na viungo vya binadamu ambavyo ni sehemu tano za siri za mwanamke (uke), mafuvu mawili ya binadamu na chuchu tano za mwanamke, kinyume na sheria.

Mashtaka mengine ni kukutwa na viungo vya uzazi vya wanyama mbalimbali kinyume na sheria.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira alitoa masharti ya dhamana ambayo mshtakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria watakaosaini bondi ya Sh5 milioni kila mmoja.

Pia mshtakiwa huyo anatakiwa kusaini bondi ya sh5 milioni na asitoke nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha mahakama.

Mshatikwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na hivyo kurudishwa rumande.

Hakimu Rugemalira aliahirisha keshi hiyo hadi Julai 5,2022 itakapoitwa kusomewa hoja za awali.

error: Content is protected !!