Taasisi ya Saratani ya Ocean Road imetakiwa kutomrudisha mgonjwa yeyote wa Saratani nyumbani kwa sababu ya kutokuwa na pesa za matibabu.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akizindua bodi ya udhamini ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
“Ni vyema mgonjwa anayefika kwenye hospitali akapewa matibabu kwanza kisha tutaona namna ya kufanya”.
Aidha, Waziri Ummy ameahidi kuipatia taasisi hiyo kiasi cha shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya kununua mashine ya CT-SCAN ili kuboresha huduma za matibabu pamoja na kumpunguza foleni kwa wagonjwa.
“Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatekeleza kwa vitendo na inatatua changamoto za wananchi na kuhakikisha huduma bora zinatolewa hapa hapa nchini.