Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini zimesaini mkataba wa Mashirikiano ya kufundisha lugha ya Kswahili katika ngazi Elimu ya Msingi nchini Afrika Kusini.
Makubaliano hayo yamesainiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknololojia Prof. Adolf Mkenda kwa niaba ya Tanzania na Waziri wa Elimu Msingi Angelina Motshekga kwa niaba ya Serikali ya Afrika Kusini wakati wa shamrashamra za Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7, 2022 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Leo tunaingia rasmi makubaliano ya mashirikiano na Afrika Kusini kufundisha Kiwahili katika shule za msingi, Rais wetu aliagiza tutie saini leo makubaliano haya katika Siku ya Kiswahili Duniani, tutakwenda kufundisha Kiswahili Afrika Kusini,” amesema Prof. Mkenda.
Viongozi hao wamekubaliana mara baada ya kusaini mkataba huo wataalamu kutoka pande zote mbili watakutana hapa nchini kuweka mpango kazi wa namna ya kutekeleza mkataba huo.
“Tutavuka mto Ruvuma, mto Zambezi na mto Limpopo kwenda kufudisha Kiswahili katika shule za msingi mchini Afrika Kusini" amesisitiza Prof. Mkenda.
Ili kutekeleza Wizara za Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watashiriki kwa kuwa wanadhana na sekta ya Utamaduni ambayo ndiyo yenye kusimamia lugha ya Kiswahili.
Naye Waziri wa Elimu Msingi Angelina Motshekga asema Afrika Kusini inaungana na Tanzania kujivunia lugha ya Kiswahili.
“Kiswahili ni zaidi ya lugha, tumejipanga kuwa sehemu ya lugha Kiswahili nchini kwetu,” amesema Waziri Motshekga.
Aidha, amesema kuwa Kiswahili ni kiunganishi muhimu cha kuimarisha uhusiano mzuri uliyopo kati ya nchi zote mbili ili kuimarisha historia za nchi hizo.