TCU yafungua dirisha la udahili vyuo vikuu

HomeKitaifa

TCU yafungua dirisha la udahili vyuo vikuu

Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) imefungua dirisha la udahili kwa masomo ya shahada ya kwanza mwaka wa masomo 2022/2023, kuanzia jana Julai 8 hadi Agost 5 mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Tume, Prof Charles Kihampa, amewataka waombaji wote kupata taarifa sahihi za udahili kwenye tovuti ya TCU au kutoka vyuo vikuu vilivyoruhusiwa kufanya udahili.

“Maombi yanahusu makundi matatu ya waombaji ambayo ni wenye sifa stahiki za Kidato cha Sita, wenye sifa stahiki za Stashahada au sifa linganifu na wenye sifa stahiki za Cheti cha Awali cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,” amesema.

Ili kufahamu sifa stahiki kwa makundi hayo, waombaji wanaelekezwa kusoma vigezo vilivyooneshwa katika vitabu vya mwongozo vya TCU mwaka 2022/2023, vinavyopatikana katika tovuti ya Tume, amesema.

Waombaji wenye vyeti vilivyotolewa na mabaraza ya mitihani nje ya nchi ni lazima waviwasilishe Baraza la Mitihani la Tanzania, kwa vyeti vya Elimu ya Sekondari, au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi, kwa vyeti vya Stashahada, ili kupata ithibati ya ulinganifu wa sifa zao kabla yakutuma maombi ya udahili.

error: Content is protected !!