Bodi ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeridhia mkopo wa dola za Marekani bilioni 1.046 (Takriban Tsh. 2.422,536,000,000) kwa Tanzania katika kipindi cha miezi 40 kusaidia kukabiliana na athari za vita ya Urusi na Ukraine. Kiasi cha dola za Marekani milioni 151.7 kitatolewa mara moja.
Taarifa ya IMF inaeleza kuwa, vita hiyo inakwamisha uchumi wa Tanzania kuimarika kufuatia mlipuko wa Uviko-19, hivyo kuleta changamoto zaidi katika maendeleo.
Tanzania ilishapokea mkopo wa dola milioni 567 mwishoni mwa 2021 ili kukidhi mahitaji yake ya dharura wakati mlipuko wa virusi vya corona ulipoathiri maendeleo ya kiuchumi, hususan sekta ya utalii kwa kiasi kikubwa.