Kagongwa kupata umeme

HomeKitaifa

Kagongwa kupata umeme

Waziri wa Nishati, January Makamba amemuagiza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Grace Ntungi kuhakikisha ndani ya wiki mbili kuanzia jana July 18 2022 wale wote waliotuma maombi ya kuunganishiwa umeme wawe tayari wameunganishwa na huduma hio.

Waziri Makamba ameyasema hayo alipozungumza na Wananchi wa Kata ya Kagongwa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga baada ya kuwepo kwa kero za kuchelewa kuunganishiwa umeme baada ya hatua za maombi kukamilika.

Waziri Makamba amesema “Ndani ya wiki mbili, wale wote wenye maombi ya Umeme na wamekamilisha vigezo vyote wawe wameunganishiwa umeme, kwa sasa vifaa vipo hivyo sitaki kusikia Kagongwa bado wana shida ya umeme”

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Grace Ntungi amesema kuanzia wiki ijayo wataanza kuongeza transforma kwenye maeneo maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya umeme na tayari wameanza survey wiki iliyopita na inaendelea na wiki hii na kuahidi mpaka tarehe 26/07/2022 watakua wamemaliza ahadi zote za umeme Kagongwa. 

 

SOURCE: MILLARDAYO

 

error: Content is protected !!