Kosa la jinai kupiga picha na karani wa sensa

HomeKitaifa

Kosa la jinai kupiga picha na karani wa sensa

Serikali imeonya makarani wa sensa ya watu na makazi waache kupiga picha na wananchi wanapoifanya kazi hiyo.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk Albina Chuwa alisema ni kosa la jinai kwa makarani kupiga picha wakiwa katika kaya za watu na kuzitumia katika mitandao ya kijamii.

Dk Chuwa aliyoa onyo hilo alipozungumza na waandishi wa habari wakati akikagua maendeleo ya shughuli hiyo mkoani Iringa.

“Kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu sura ya 351 ni kosa kumrekodi video au kumpiga picha mwananchi ambaye unamhoji ili kupata taarifa zake… kwenda kwenye kaya ya Mtanzania mwenzako na kurekodi mambo yaliyopo kwenye kaya yake yawe mazuri au mabaya haikubaliki na kinyume na sheria,” alisema.

Dk Chuwa alisema adhabu ya kufanya hivyo ni kifungo cha miezi sita jela au faini ya sh milioni mbili au vyote kwa pamoja.

 

 

 

error: Content is protected !!