Serikali kuja na bei elekezi ya mifugo

HomeKitaifa

Serikali kuja na bei elekezi ya mifugo

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema serikali ipo kwenye mchakato wa kushirikisha wadau wa sekta ya mifugo kupanga bei elekezi za kuuzia mifugo katika minada.

Uwapo wa bei elekezo kutawezesha wafugaji na wafanyabiashara kuuza mifugo yao kwa bei ambayo wao watakuwa wameshiriki kuipanga. Alitoa kauli hiyo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mnada wa kimataifa wa Buzirayombo unaojengwa wilayani Chato, mkoani Geita mwishoni mwa wiki.

Alisema suala la kuwa na bei elekezi, serikali inalifanyia kazi na tayari wataalamu walishaandaa na hatua iliyopo sasa ni ya kuwashirikisha wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo ili kwa pamoja waweze kukubali- ana na kuja na bei ambayo itakuwa imeridhiwa na pande zote.

“Bei elekezi ikitoka ndio itakuwa mahali pa kuanzia na kwenda juu, hivyo tunalifanyia kazi suala hilo na muda sio mrefu tutatoa mwelekeo wa jambo hilo,” alisema.

error: Content is protected !!