Rais Samia : Watanzania wekezeni Msumbiji

HomeKimataifa

Rais Samia : Watanzania wekezeni Msumbiji

Rais Samia Suluhu amewataka Watanzania wanaoishi na kufanya biashara nchini Msumbiji kutumia fursa ya ushirikiano wa nchi hizo mbili kuwekeza kwa faida ya pande zote mbili.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika ofisi za Manispaa ya Jiji la Maputo nchini Msumbiji jana akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu nchini humo.

Akiwa hapo, Rais Samia alipata heshima ya kukabidhiwa funguo ya Jiji la Maputo kama ishara ya heshima na ushirikano baina ya Tanzania na Msumbiji.

Alisema Serikali ya Tanzania inajua wazi kuna Watanzania wengi wanaoishi Msumbiji, hivyo yeye na Rais Filipe Nyusi wamekubaliana kuwaeleza raia wao kushirikiana kwa faida ya nchi hizo mbili.

“Sisi Watanzania tunajua kwamba kuna Watanzania wengi wanaoishi na kufanya biashara Maputo, nikiwa na kaka yangu Nyusi tulikubaliana kuwaeleza watu wetu kushirikiana kufanya biashara na kuwekeza kwa manufaa ya nchi zetu,” alisema Rais Samia.

 

error: Content is protected !!