Tanzania kuchangia bilioni 2.3 Global Fund

HomeKimataifa

Tanzania kuchangia bilioni 2.3 Global Fund

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango a,etoa mwito kwa mataifa duniani kuungana katika kutoa mchango kwa Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) ufikie lengo la kukusanya dola za Marekani bilioni 18.

Dk Mpango alisema hayo juzi jijini New York nchini Marekani alipohutubia Mkutano wa Saba wa Kuiwezesha Global Fund.

Katika mkutano huo, Tanzania imeahidi kuchangia dola za Marekani milioni moja (Sh bilioni 2.3) katika Gloabl Fund ili kuwezesha kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.

Dk Mpango alisema migogoro imepunguza juhudi za kurejesha uchumi wa nchi nyingi ulioathrika na janga la Covid-19 na kuongeza changamoto katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Alisema Tanzania inathamini ushirikiano wa kihistoria uliopo baina yake na Gloabl Fund ambao umekuwa na matokeo chanya na kuwezesha kupunguza idadi ya vifo vya Ukimwi, KIfua Kikuu na Malaria.

error: Content is protected !!