Mradi wa gesi LPG kuanza mwaka huu

HomeKitaifa

Mradi wa gesi LPG kuanza mwaka huu

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema mradi wa kuchakata gesi asilia mita za ujazo bilioni 4.6 na bidhaa nyingine ya gesi ya kupikia (LPG), unatarajia kuanza nchini mwaka huu.

Pia, amebainisha serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha majadiliano yote ya msingi kuhusu mradi huo wa kuchakata na kusindika gesi asilia yanakamilika ifikapo Desemba, mwaka huu.

Waziri Makamba alisema hayo jana akiwa na Balozi wa Tanzania katika Nchi za Nordic, Grace Olotu na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen, baada ya kushiriki katika warsha ya mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia na gesi ya kupikia.

Alisema mradi huo unaotarajia kufanyika nchini, pia upo kaskazini mwa Norway ambako warsha hiyo ilikuwa sehemu ya kujifunza mafanikio ya kuchakata gesi asilia.

“Pia tumekutana na Watanzania wanaofanya kazi katika mradi huo na kupata nafasi ya kujadili maandalizi ya mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia Tanzania wenyewe thamani ya sh. Trilioni 70 utakaofanyika mkoani Lindi,”alisema Waziri Makamba.

Aidha, Waziri Makamba aliwahakikishai Kampuni ya Equinor na washirika wake, Tanzania itaendelea kushirikiana nao ili kuhakikisha majadiliano ya msingi yanakamilika.

error: Content is protected !!