Rais Samia atoa bilioni 2.7 kwa ajili ya tiba asili

HomeKitaifa

Rais Samia atoa bilioni 2.7 kwa ajili ya tiba asili

Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa sh. Bilioni 2.7 ili zitumike kufanya utafiti katika sekta ya tiba asili nchini.

Taarifa ya kutolewa kwa fedha hizo imkeuja zikiwa zimepita siku mbili tangu utafiti ili kujua sababu ya vijana kukosa lishe bora, hatua inayowafanya baadhi yao watumie supu ya pweza na ‘vumbi la kongo’.

Akizungumza wakati akizindua Kituo cha Tiba Asili na Tiba Jumuishi Afrika, kilichopo Kijiji cha Ngarenanyuki, Arumeru mkoani Arusha, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, alisema Rais Samia ana nia ya dhati ya kuboresha sekta ya tiba asili nchini.

“Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ametoa sh. Bilioni 2.7 za utafiti katika eneo la tiba asili. Rais ana nia ya dhati ya kuendeleza tiba asili,”

“Tuwatumie hawa (Kituo cha Tiba Asili Jumuishi Afrika) kuwajengea uwezo watu wetu ili tuwe na tiba asili kama hii katika hospitali zetu,” alisema Dk. Mollel.

 

error: Content is protected !!