Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,amewapongeza wahitihu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam waliohitimu leo Novemba 30, 2022.
Rais Samia Suluhu ametoa pongezi hizo wakati wa hotuba yake katika Mahafali hiyo ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na kuwataka wahitimu hao wakayafanyie kazi yale yote walifundishwa pindi wapo chuoni hapo.
“Mlifanya bidii kubwa…mlipambana kufa na kupona hadi kufuzu na kufikia hapa katika mahafali hongereni sana, mlihakikisha kuwa mnakwenda maktaba na mmesoma vitabu mlivyoelekezwa, mmekwenda maabara na karakana, mliudhuria mijadala na wengine mlijiunga na makundi sogozi sio kuchapa umbea bali kutafuta elimu,
“Sasa dunia yote inawasubiri mkayaweke kwa vitendo mliyofunzwa hapa kutoka kwa wahadhiri na wanataaluma,” amesema Dkt. Samia.