Bidhaa za Tanzania kutotozwa ushuru Uingereza

HomeKitaifa

Bidhaa za Tanzania kutotozwa ushuru Uingereza

Serikali ya Uingereza imefungua milango kwa bidhaa za Tanzania kulifikia soko la nchi hiyo bila kutozwa ushuru.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara anayehusika na Uwekezaji, Ally Gugu, Balozi wa Uingereza nchini, David Concar na Mwakilishi Maalumu wa masuala ya biashara wa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa Tanzania, Lord Walney walisema hayo Dar es Salaam.

Waliwaeleza waandishi wa habari kuwa Serikali ya Uingereza kupitia ubalozi wake nchini kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, zilifanya kongamano lao la pili la mwaka la biashara jijini Dar es Salaam.

Gugu alisema Uingereza ni moja ya wawekezaji wakubwa wanaofanya biashara na kuwekeza nchini na mara nyingi hushika ama nafasi ya kwanza au ya pili kwa uwekezaji nchini.

Amesema ili kuimarisha ushirikiano huo wa kibiashara na uwekezaji, Tanzania na Uingereza ziliona kuna haja ya kuanzisha kongamano hilo ili kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kujadili fursa, masuala ya kisera na changamoto wanazokutana nazo.

Alisema maoni na mapendekezo yatakayopatikana yataiwezesha serikali kuona namna kuboresha sera, sheria na taratibu zake ili kuvutia zaidi wawekezaji na wafanyabiashara hususani kutoka Uingereza.

error: Content is protected !!