Uhaba wa malisho chanzo cha bei ya nyama kupaa

HomeKitaifa

Uhaba wa malisho chanzo cha bei ya nyama kupaa

Meneja wa Shughuli za Masoko wa Bodi ya Nyama nchini, John Chasama amesema uhaba wa ng’ombe unaosababishwa na kukosekana kwa malisho kumepelekea bei ya nyama kupaa.

Katika kipindi cha mapitio, bei ya ng’ombe wa daraja la kwanza ilipanda kutoka Sh 1.97 milioni wiki iliyopita hadi sh 2.1 milioni wiki hii, kulingana na bodi ya nyama nchini.

Chasama alisema bei ya ng’ombe wa daraja la pili ilipanda kutoka Sh1 milioni wiki iliyopita hadi kufikia sh1.15 milioni wiki hii.

“Ukame umechangia kuongezeka kwa bei ya ng’ombe wenye afya sasa hawapatikani. Huwezi kuuza ng’ombe wasio na afya sokoni kwa sababu hata nyama yao haiwezi kuwa znuri kwa hivyo lazima uende mbali kutafuta wenye afya.”

Kupanda kwa bei ya ng’ombe ilibidi kulazimu walaji wa nyama kutoboka zaidi mifuko ili kuoata bidhaa hiyo.

Bei ya ng’ombe katika Soko la Pugu kwa wiki inayoishia Novemba 23, imepanda kwa asilimia 6.5 ikilinganishwa na wili iliyopita, hali iliyosababisha nyama kuuzwa kwa bei ya juu.

error: Content is protected !!