Namba za kupiga kuhesabiwa sensa

HomeKitaifa

Namba za kupiga kuhesabiwa sensa

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022,Mheshimiwa Anne Makinda amesema asilimia 93.45 ya kaya zote Tanzania zilikuwa zimehesabiwa hadi kufikia asubuhi ya saa 2 jana Agosti 29,2022.

Mheshimiwa Makinda amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya Sensa ya Watu na Makazi ambapo ilianza Jumanne ya Agosti 23, 2022.

Makinda ametoa muongozo kwa wananchi ambao watakuwa hawajahesabiwa mpaka kufikia juzi jioni kuwa bado wana nafasi ya kuhesabiwa akitoa utaratibu ikiwemo kwenda kwenye ofisi za serikali za mitaa wanakoishi.

Mwananchi unashauriwa uende moja kwa moja kwenye ofisi za Serikali za mitaa na onana na mwenyekiti au mtendaji wa mtaa unaoishi na hakikisha unawachia namba ya mawasiliano ili karani akufuate ulipo na kuanza kazi ya kukuhesabu.

error: Content is protected !!