Maboresha katika Bandari ya Tanga yaanza kuleta matunda

HomeKitaifa

Maboresha katika Bandari ya Tanga yaanza kuleta matunda

Bandari ya Tanga kwa mara ya kwanza imepokea meli ambayo imebeba mzigo wa magari pamoja na shehena nyingine za mizigo kutoka nchini China.

Meli hiyo ijulikanayo kwa jina la Della, ilipakia shehena ya mizigo katika Bandari ya Zhanjiangang iliyoko Shanghai nchini China na kusafirisha mizigo katika Bandari mbalimbali ikiwemo ya Tanga.

Akizungumza wakati wa upokeaji wa shehena hiyo ya mizigo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amesema ujio wa meli kubwa za mizigo inatokana na maboresho makubwa yaliyofanyika ya ujenzi wa gati mpya yenye urefu wa mita 450.

“Hii bandari ndio moyo wa uchumi wa Mkoa wa Tanga, hivyo huu ni mwanzo tuu wa ujio wa meli kubwa kwani tutaendelea kuvunja rekodi Kila mara na niwaombe wafanyabiashara kuitumia bandari ya Tanga kwa ajili ya uhakika wa usafirishaji wa mizigo, “amesema Kindamba.

error: Content is protected !!