Kutokana na Hotuba ya Wazari wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, iliyosomwa na Waziri Nape Nnauye imeonesha kuwa Sekta ya Mawasiliano imeendelea kukua, huku takwimu zikionesha kuwa;
- Laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 55.7 Mwezi Aprili,2022 hadi kufikia milioni 62.3 mwezi Aprili,2023.
- Watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka milioni 29.9 Mwezi Aprili,2022 hadi milioni 33.1 Mwezi Aprili,2023.
- Watumiaji wa huduma za kutuma na kutoa pesa kwa njia ya mtandao wa simu wameongezeka kutoka milioni 35.7 mwezi Aprili,2022 hadi milioni 44.3 mwezi Aprili,2023.
- Watoa huduma wa huduma za ziada (Application Services and Value Added Services) wamefikia 141 ukilinganisha na watoa huduma 102 Mwezi Aprili, 2022 (ongezeko la asilimia 38).
- Watoa huduma wa Miundombinu ya Mawasiliano wamefikia 23 ukilinganisha na watoa huduma 22 Mwezi Aprili, 2022 (hii ni sawa na ongezeko la asilimia 4.5)