Mahakama Kuu nchini Tanzania hii leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa inapinga mkataba (IGA) wa uwekezaji wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na falme ya Dubai.
Kesi hiyo iliyofunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Mbeya na walalamikaji wanne ambao walidai mkataba huo unaenda kinyume na matakwa ya Katiba.
Akisoma Hukumu hiyo Jaji Dastan Ndunguru amesema baada ya jopo la majaji wa tatu kusikiliza pande zote mbili mahakama imeamua kuwa hoja zote sita hazina mashiko hivyo kuamua kuwa Mkataba wa IGA hauna dosari za kufanya usitekelezwe.
Misingi minne ilianishwa kwenye malalamiko hayo ni:
- Mkataba kuridhiwa bila kuutoa kwa uma na muda wakushiriki kwa wananchi.
- Mkataba wa IGA uliosainiwa unakiuka sheria.
- Mkataba ni kinyume na maslahi ya umma na rasilimali za umma.
- Mkataba unahatarisha usalama wa nchi kwa baadhi ya vifungu.
Akiongea na waandishi wahabari Wakili wa walalamikaji Bonifasi Mwabukusi amesema wanajipanga kwenda kukata rufaa kwani hawajakubaliana na uamuzi wa mahakama.