Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kukasilishwa na mwenendo wa mikutano ya hadhara miezi kadhaa tangu airuhusu tena tangu ya kuwa imefungiwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Katika hotuba yake wakati wa Mkutano Maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Rais Samia amesema iliruhusu mikutano ya hadhara kwa lengo la kuwezesha vyama kuzungumza na kukua.
“Tulitaka vyama vizungumze, wananchi wasikie sera zao, mada zao, mipango yao ili vyama vikue na virudishe watu wao walio wapoteza … vyama viwe madhubuti tukienda kwenye uchaguzi kila chama kimejijenga vya kutosha,” amesema Rais Samia.
Amesema serikali haikuruhusu mikutano ya hadhara ili watu wakavunje sheria, kutukana, kukashifu, kuchambua dini za watu. “Lakini sishangai haya yanatokea kwa sababu ya kuzungumza hakuna.