Rais Samia anatekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo

HomeKitaifa

Rais Samia anatekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo

Rais Samia Suluhu amegawa boti 34 kati ya 160 zilizonunuliwa na Serikali kwa wavuvi na wakulima wa mwani ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi 2022-2025 inayoielekeza serikali kuweka mazingira wezeshe kwa wananchi waweze kunufaika na rasilimali zao pamoja na kukuza uchumi wa buluu nchini.

“Juhudi hizi tunazozifanya ni uthibitisho tosha wa umakini wa serikali yenu katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi,” amesema Rais Samia

Amegawa boti hizo zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 280 wakati akiweka jiwe la msingi katika Bandari ya Uvuvi Kilwa na kusema Serikali imefanya tukio muhimu la kihistoria kwa kujenga bandari hiyo ya kwanza ya uvuvi nchini.

” Boti hizi 160 zimetolewa kwa mkopo wa masharti nafuu na unalenga kutoa ajira na kuongeza kipato cha jamii. Boti ndogo zitatumiwa na akina mama kulima mwani na kubeba mizigo, na zile kubwa zinakwenda kwenye kina cha maji marefu, ” ameeleza Rais Samia.

Rais Samia amesema kuwa serikali haitarajii boti hizo kuleta ugomvi katika vikundi vya wakulima na wavuvi bali zitumike kuimarisha uchumi wao.

 

 

error: Content is protected !!