Rais Samia aandika historia Kilwa

HomeKitaifa

Rais Samia aandika historia Kilwa

Historia imeandikwa mkoani Lindi na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu katika sekta ya uvuvi baada ya kuweka jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko ambayo haijawahi kuwepo tangu nchi ipate uhuru.

Kukamilika kwa bandari hiyo kutawezesha meli za uvuvi zinazovua katika ukanda wa Uchumi wa Bahari ya Tanzania na Bahari Kuu kutia nanga na kushusha samaki wanaolengwa na wale wasiolengwa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.

Aidha, bandari hiyo itachochea uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya kuchakata samaki na miundombinu ya uhifadhi wa mazao ua uvuvi, kuimarika kwa biashara ya mazao ya uvuvi yanayokwenda nje ya nchi kutoka tani 40,721.53 hadi tani 52,937.99 na hivyo kuchangia takriban asilimia 10 ya pato la taifa ifikapo mwaka 2036.

error: Content is protected !!