Rais Samia awasogezea huduma bora za afya wananchi wa Lindi

HomeKitaifa

Rais Samia awasogezea huduma bora za afya wananchi wa Lindi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Septemba 2023 anatarajia kufungua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.

Hospitali hiyo hadhi yake inafanana kabisa na Hospitali zingine kubwa Kama Muhimbili ya Dar es salaam, itatoka huduma za wagonjwa wa nje, wagonjwa wa dharura, huduma za radiolojia na itamaliza rufaa za wagonjwa kwenda Dar es Salaam na mikoa mingine kwa ajili ya huduma za CT Scan.

Aidha wananchi wa Mkoani humo wamefurahishwa sana na jitihada hizo za Mhe.Rais kuwajengea Hospitali hiyo kubwa na kupunguza kero waliyokuwa wanaipata hapo mwanzo kusafiri nje ya mkoa kupata huduma ya matibabu kwa yale magonjwa mugu.

error: Content is protected !!