Rais Samia kufungua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi kesho

HomeKitaifa

Rais Samia kufungua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi kesho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 19 Septemba 2023 anatarajia kufungua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati akisalimia wananchi wa Mtama Mkoani Lindi wakati wa ziara ya Rais Mkoani humo.

Dkt. Mollel ameeleza kuwa hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi baada ya kufunguliwa itaanza kutoa rasmi huduma za wagonjwa wa nje (OPD), Huduma za wagonjwa wa dharura (EMD), huduma za Radiolojia na itamaliza Rufaa zote za huduma za CT Scan baada ya kuanza kutolewa mkoani Lindi hivyo kuwarahisishia wananchi kutosafiri kwenda Dar es Salaam na Mikoa mingine ya jirani.

 

error: Content is protected !!