‘My Name’ Filamu itakayochangamsha wikiendi yako

HomeBurudani

‘My Name’ Filamu itakayochangamsha wikiendi yako

Katika filamu hii  ya “My name”, (Jina langu kwa tafsiri ya Kiswahili), tunakutana na binti mrembo Yoo Ji Woo, ambaye katika maisha yake amekuwa akilelelewa na Baba yake tu. Kwa jinsi Baba yake alivyokuwa akimpenda sana, basi Jiwoo anaweza kujiita “Dad’s daughter” kama vile ambavyo wadada hujigamba.

Maisha ya Jiwoo na Baba yake siyo mazuri sana, kwani Baba yake hakuwa na kazi rasmi ya kuwaingizia kipato zaidi ya kuwa mtu anayejihusisha na kazi haramu, lakini baadae maisha ya Jiwoo yanakuja kubadilika siku ambayo anatimiza miaka 17. Siku hiyo Baba yake anaaga Dunia kwa kupigwa risasi tena mbele ya macho yake.

Maisha anayoanza kuishi Jiwoo baada ya Baba yake kuuwawa ndiyo yanayoipatia filamu hii jina la ‘My Name’, maana Jiwoo anahakikisha Korea Kusini yote inalijua jina lake. Dada huyu anakuwa rasmi ‘gangstar’ kama baba yake na zaidi  anakuwa ni ‘gangstar’ asiye na huruma wala kumuogopa yeyote.

> Maid – filamu itakayonogesha wikiendi yako

Choi Mu-jin, kiongozi wa genge kubwa la wahuni wanaojihusisha na kuuza madawa ya kulevya anamsajili rasmi Jiwoo katika genge lake na kuahidi kufanya lolote analoweza ili kumsaidia kulipiza kisasi cha kifo cha baba yake.

Hasira inayowaka kwenye moyo wa Jiwoo  ni zaidi ya moto wa kichaka. Anapambana kujiunga na jeshi la Polisi akisaidiwa na Mujin mpaka anafanikiwa kujiunga na jeshi hilo. Kibarua chake siyo tu kumuua adui yake bali kupeleka taarifa zote za Jeshi la Polisi kwa Mujin.

Safari ya kulipiza kisasi iliyojaa chuki na hasira itamfikisha wapi Jiwoo? Ni nani mhusika halisi wa kifo cha Baba yake?. Majibu yako katika filamu ‘My Name’.

error: Content is protected !!