Rais Samia anavyoipambania lugha ya Kiswahili

HomeKitaifa

Rais Samia anavyoipambania lugha ya Kiswahili

Rais Samia Suluhu amewasihi wajumbe wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutumia lugha ya Kiswahili na pia kuharakisha mchakato wa kuifanya iwe miongoni mwa lugha nne za zinazotumika kwenye Jumuiya hiyo.

Akizungumza kwa lugha ya kiswahili katika Mkutano wa 42 wa SADC uliofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Rais Samia amezisihi pia nchi hizo kuwekeza kwenye ‘Uchumi Buluu’.

Aidha, Rais Samia alizungumzia uwiano wa kijinsia waliokubaliana katika ukanda huo na kusema Tanzania imejitahidi kutoa fursa kwa wanawake hasa katika nafasi za uongozi za kimkakati.

Miongoni mwa nafasi hizo za uongozi serikalini na bungeni ni pamoja na za uwaziri wa Ulinzi, Mambo ya Nje, Uwekezaji, Utalii pamoja na nafasi ya Spika wa Bunge.

Rais Samia leo atafanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini DRC ambapo pamoja na mambo mengine, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa DRC, Felix Tshisekedi.

 

error: Content is protected !!