Rais Samia: Lengo la BBT ni kupunguza umaskini na kutunza mazingira

HomeKitaifa

Rais Samia: Lengo la BBT ni kupunguza umaskini na kutunza mazingira

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema lengo la Programu ya Jenga Kesho iliyobora (BBT) ni kupunguza umaskini lakini pia kutunza mazingira.

Amesema hayo kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula, Ngurdoto uliofanyika Mkoani Arusha leo tarehe 23 Novemba, 2023.

“Lengo letu ni kuongeza uzalishaji lakini kupunguza umaskini wakati huohuo tunatunza mazingira. Kwa sababu kutunza mazingira bila kupunguza umaskini tutakuwa tunafanya kazi bure. Kwahiyo tunatunza mazingira wakati huohuo tunapunguza umaskini.” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ameitaka sekta binafsi kushiriki katika kuunga mkono mradi huo wa kuinua vijana na wanawake kupitia kilimo.

“Kazi ya serikali ni kuwapa vijana ardhi lakini pia mafunzo. Sasa sekta binafsi tunaitaka iingie kwenye kutoa fedha, lakini pia mitambo kufanya kilimo chetu kiwe cha kisasa.” amesema Rais Samia.
error: Content is protected !!