Hatua ya kutaka kurekebisha sheria ya mahari pamoja na ndoa za mitala ya mwaka 1987 nchini DRC imezua gumzo kubwa kwa watu wa Jamhuri ya Congo.
Muswada uliowasilishwa mwezi Juni Bungeni na Waziri Mkuu Daniel Mbau unaazimia kufanya marekebisho ya kutaka mwanaume anayetaka kuoa awe na kiwango maalumu cha mahari.
Waziri Mkuu akiwa anasoma mswada huo amesema kuwa wanaume waishio vijijini watalipa dola 200 na dola 500 kwa waishio mjini.
Inaripotiwa kwamba, sasa hivi wapo wazazi jijini Kinshasa wanaohitaji zaidi ya dola 5000 kama mahari ya watoto wao. Gharama hiyo inaweza kuongezeka zaidi kulingana na kiwango cha elimu. Waziri Mkuu amesema kuwa mahari nchi Congo imekuwa biashara ambayo imenza kuleta matatizo kwenye jamii.
Raia wengi wa Congo wamesema hakuna haja utamaduni huo. Hatua ya kukata kubadili sheria hiyo imekuja baada ya wazazi wengine kuanza kudai vitu kama tiketi za ndege.