Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu amesema serikali yake anayoiongoza inatekeleza kwa vitendo maagizo yote yaliyomo katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mbinga baada ya kuzindua Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
“Ndugu zangu wa Mbinga kukamilika kwa jengo hili ni kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo imetutaka tujenge majengo ya halmashauri ili kutoa nafasi ya kuhudumia vizuri wananchi lakini pia kukuza utawala bora” amesema Rais Samia.
Aidha, Rais Samia aliwasihi watumishi walitunze jengo hilo liendelee pamoja na kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora.
Rais Samia yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ambapo leo ni siku ya pili ya ziara hiyo itakayomalizika Septemba 28,2024.