Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema uamuzi wa kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za Shilingi ya Tanzania zilizoidhinishwa kutumika na benki hiyo mwaka 1985 hadi 2003 na noti za shilingi 500 iliyoanza kutumika mwaka 2010, hauna athari za kiuchumi na benki hiyo haina mpango wa kuleta haina matoleo mapya kwa sasa.
Imesema kuziondoa haina maana kuwa zimeshuka thamani bali ni utaratibu wao wa kawaida kwa mujibu wa sheria kufanya hivyo pale inapoona haja ya kufanya hivyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sarafu wa BoT, Ilulu Ilulu alisema hayo Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango wa kuondoa noti hizo za zamani kwenye mzunguko wa sarafu.
View this post on Instagram