Wafanyabiashara wakimbilia fursa SGR

HomeKitaifa

Wafanyabiashara wakimbilia fursa SGR

BAADHI ya wafanyabiashara wamejitokeza kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kutaka wawe wanasafirishiwa mizigo yao kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma wakati Treni ya Kisasa (SGR) ya mizigo itakapoanza.

Novemba mwaka jana, TRC ilipokea mabehewa 264 kutoka China yanakotengenezwa kuanza kwa safari za treni ya mizigo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema ma behewa hayo ni kati ya mabe hewa 1,430 ambayo yanatakiwa kutengenezwa kwa mujibu wa mkataba kati ya serikali kupitia TRC na CRRC ya China.

“Habari njema ni kwamba tayari baadhi wafanyabiashara wameshakuja kutaka mizigo yao waipokelee Dodoma… wote tunajua treni ya mizigo ndio itakayotuingizia mapato zaidi,” alisema Kadogosa.

Alisema muda wowote kuanzia sasa mabehewa hayo yataanza kufanyiwa majaribio yatakayochukua takribani miezi miwili kabla ya kuruhusiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) kuanza biashara ya usafirishaji mizigo.

Kwa mujibu wa Kadogosa, mabehewa 200 kati ya 264 ni ya kubeba makasha na mabehewa 64 ni ya mizigo isiyofungwa.

“Tunajua tuna treni za abiria lakini haziingizi mapato makubwa kama ilivyo kwa treni za mizigo, fursa ziko nyingi, naamini zitakapoanza itakuwa mtatuzi wa mambo mengi,” alisema Kadogosa.

Kwa mujibu wake, treni hizo zinatarajiwa kuanza usafirishaji kati ya Machi na Aprili mwaka huu. Tanzania ilianza usafiri wa SGR Juni na Agosti mwaka jana kwa treni za abiria kutoka Dar es Salaam – Morogoro – Dodoma na mpaka sasa TRC imeshasafirisha zaidi ya abiria milioni 1.4.

Usafiri wa treni ya mizigo unatarajiwa kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara wengi kwani sasa watafikisha mizigo yao kwa haraka zaidi kwa vile usafiri wa lori unatumia muda mwingi njiani

error: Content is protected !!