Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM wameshinikiza chama hicho kuwapitisha kwa kauli moja Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kuwania tena nafasi hizo katika uchaguzi wa mwaka huu.
Baada ya mapendekezo hayo waliyoyatoa wakati wa michango yao baada ya kutazama na kusikiliza utekelezaji wa llani ya chama hicho Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akashauri ili jambo hilo lifanyike na liwe kisheria lazima liandaliwe Azimio maalum.
Rais Samia ameagiza sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM kukaa ili kuandaa azimio hilo ili lipitishwe leo na wajumbe wa
Mkutano Mkuu.