Hizi ndio tozo zilizofutwa na serikali

HomeKitaifa

Hizi ndio tozo zilizofutwa na serikali

Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba amesema baada ya kupitia upya tozo za miamala ya fedha serikali imeamua kupunguza na kufuta baadhi ya tozo huku akitangaza utaratibu mpya ambao unatarijiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu.

Maamuzi yaliyofikiwa baada ya kupitia tozo ni kama yafuatayo 

  1. Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu pande zote.
  2. kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja.
  3. Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki nyingine kwenda benki nyingine.
  4. Kutowahusisha wafanyabiashara kama ilivyokuwa kwenye kanuni za sasa.
  5. Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki ya ATM kwenye miamala yenye thamani ya chini ya elfu thelathini .
  6. Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50 kufuatana na kundi la miamala.

Sambamba na hatua hiyo, Serikali imefuta utaratibu wa kodi ya zuio inayotokana na pango kukusanywa na mpangaji na badala yake jukumu hilo linarejeshwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa utaratibu utakao bainishwa kwenye kanuni. 

Mwigulu amesisitiza pia kuwa kodi ya zuio ya pango siyo ya mpangaji bali inapaswa kulipwa na mpangishaji ambaye ndiye anapokea mapato kutokana na uwekezaji au biashara ya kupangisha. 

 

error: Content is protected !!