Busara yatumika kupunguza faini ya Manara

HomeKitaifa

Busara yatumika kupunguza faini ya Manara

Kamati ya rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF leo imetangaza kumpunguzia adhabu Msemaji wa Yanga Haji Manara kutoa milioni 20 ya faini aliyotakiwa kuilipa hadi milioni 10 huku hukumu ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka miwili ikibaki palepale.

Mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya Maadili ya TFF, Richard Mbaruku amesema hii ni baada ya kupitia rufaa ya Haji Manara ambayo hata hivyo wameona haina mashiko lakini wakatumia busara ya kumpunguzia faini hiyo.

Julai 21, 2022 Haji Manara alitangazwa kufungiwa miaka miwili kujihusisha na soka pamoja na faini ya milioni 20 baada ya kukutwa na hatia ya kumkosea nidhamu Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wa mechi ya fainali ya ASFC kati ya Yanga na Coastal Union Arusha Julai 2,2022.

error: Content is protected !!