Lita ya petroli Nairobi Sh3469.94

HomeKimataifa

Lita ya petroli Nairobi Sh3469.94

Lita moja ya petroli jijini Nairobi sasa itauzwa kwa Sh3469.94 (Ksh179.30) kutoka Ksh159 katika bei mpya iliyotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli.

Katika mabadiliko hayo, lita moja ya mafuta ya petroli itauzwa kwa Sh179.30, bila ruzuku ikiwakilisha ongezeko la Ksh20.18.

Kwa upande mwingine, bei ya dizeli imeongezeka kwa Ksh25 na sasa itauzwa kwa Ksh165 jijini Nairobi.

Bei ya Mafuta ya Taa imeongezeka kwa Ksh20 kumaanisha kuwa itauza Ksh147.94 jijini Nairobi. Bei hizo ni pamoja na asilimia 8 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Kupanda kwa bei ya mafuta kunafuatia kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta kwa bidhaa za petroli na serikali ya Rais William Ruto kama ilivyojulishwa awali.

Mabadiliko ya bei ya mafuta huanza kutekelezwa mara moja.

error: Content is protected !!