UMOJA wa Mataifa umeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti zinazoonyesha kuwa kundi la waasi la M23 linapiga hatua kuelekea Kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kuuteka mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Goma.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amesema kuwa ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa, MONUSCO, umeleta taarifa kuhusu vikosi vya Rwanda kuvuka mpaka na kuelekea upande huo.
“Tunahofia sana na hali ya sasa katika Kivu Kusini, hali bado ni tete, na kuna ripoti za kuaminika kwamba M23 inasonga mbele kuelekea mji wa Bukavu,” alisema Stephane.
Hapo awali, waasi wa M23 wamesema wanataka pia kuuteka mji mkuu wa Congo, Kinshasa, baada ya Rais Tshisekedi na kuwataka vijana kujiunga na jeshi kuendeleza mapigano hayo.