Rais Samia azindua jengo la Halmashauri Bumbuli

HomeKitaifa

Rais Samia azindua jengo la Halmashauri Bumbuli

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli mkoani Tanga lililogharimu zaidi ya shilingi bilioni 3,2.

Jengo hilo lina vyumba 72 vya watumishi wa idara zote za halmashauri hiyo na kumbi mbili, moja inauwezo wa kuchukua watu 56 kwa wakati mmoja na mwingine wa watu 2,010.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa jengo hilo lililojengwa kwa kuzingatia mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum, Rais Samia amewasihi wananchi na watumishi wa umma kuhakikisha wanalilinda na kulitunza jengo hilo.

error: Content is protected !!