Rais Samia: Hata gesi iikisha endeleeni kutumia majiko haya

HomeKitaifa

Rais Samia: Hata gesi iikisha endeleeni kutumia majiko haya

RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka wanufaika wote wa mradi uliozinduliwa leo wa majiko ya Ruzuku kuendeleza matumizi majiko hayo hata pale gesi iliyogaiwa leo itakapoisha.

Rais Samia amesema tayari amezungumza na wadau wa sekta binafsi kuhakikisha kuwa vituo vya ujazaji gesi vinafunguliwa katika maeneo mablimbali hasa maeneo ya vijijini ili kurahisisha zoezi la kujaza gesi katika mitungi hiyo.

Rais Samia amesema hayo leo akiwa wilayani Muheza mkoani Tanga alipokua akizindua programu ya usambazji wa mitungi ya ruzuku 452,445 yenye thamani ya Sh bilioni 8.64.

“Mlionufaika na majiko haya ya gesi yatumieni na siyo gesi ikiisha basi mitungi inakaa kama furtniture ndani, nimeiomba sekta binafsi wakanihakikishai kwamba wnafungua maeneo huko ili mitungi hii iendelee kutumika.

Rais Samia amesema katika mitungi hiyo serikali inatoa asilimia 50 na wanunuzi watanunua kwa asilimia 50 kwa vijijini kwa kulingana sheria ya REA, huku kwa maeneo ya mjini serikali ikilipia asilimia 20 amesema mgawanyo huo unaendana na ugawaji wa maeneo kiuchumi.

Aidha, Rais Samia amesema serikali itaendelea kutunga sheria na sera rafiki zitakazoziwezesha ushiriki wa sekta binafsi katika uwezeshaji wa upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa bei

error: Content is protected !!