Dhamira ya Rais Samia juu ya makao makuu ya nchi Dodoma

HomeKitaifa

Dhamira ya Rais Samia juu ya makao makuu ya nchi Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema Rais Samia Suluhu Hassan hana makusudi ya kurejesha Makao Makuu ya Serikali jijini Dar es Salaam na kwamba ameendelea kutekeleza na kutenga fedha nyingi zaidi kwa ajili ya Dodoma kuliko maeneo mengine hapa nchini.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa, Waziri Simbachawene amesema wako watu wanafikiria Rais Samia haipendi dodoma. “Maneno haya ni kumsingizia Rais,” amesema Waziri Simbachawene. Na kuongeza, Rais Samia “anatekeleza kwa vitendo na hata kwenye bajeti hii tumeendelea kutenga bajeti. Fedha iliyoingia dodoma ni nyingi kuliko maeneo yoyote.”

Kwa mujibu wa Simbachawene, Bunge limetenga Sh bilioni 20 kwa kila wizara kwa mwaka wa fedha 2021/22 na majengo yanaendelea kujengwa.

“Serikali ilifanya maamuzi mwaka 1973 na maamuzi yamekuwa katika ilani za chama cha mapinduzi kwa miaka yote. Niipongeze serikali ya Rais Samia kuendelea kutekeleza maamuzi haya. Na hivi sasa tunavyo zungumza taasisi zote muhimu ikiwa ni pamoja na Ikulu, wizara zote zinakamilisha majengo yake muhimu.”- Waziri Simbachawene.

error: Content is protected !!