Mambo 5 yakuzingatia kabla hujachagua kava la simu

HomeElimu

Mambo 5 yakuzingatia kabla hujachagua kava la simu

Unaponunua kava la simu unatakiwa  kuzingatia zaidi usalama wa simu ambayo unalenga kuilinda ili isichubuke, isipasuke  au isiingie vumbi.         

Ili kuwa na uhakika wa kava la simu unalochagua Zingatia yafuatayo:

Zingatia malighafi

Unapochagua kava kwa ajili ya simu yako unashauriwa kununua kava iliyotengenezwa kwa malighafi yenye uwezo wa kustahimili mshtuko (shock) hasa pale simu yako inapoanguka kwenye sakafu au mahala pagumu.

Wembamba, unene

Wapo ambao hawavutiwi na  makava manene kwa sababu yanawakera mfukoni na simu zinaonekana kubwa. Lakini siri iliyopo nyuma ya unene wa kava hizo ni uwezo wa kuilinda simu yako na ajali.

Kwa mtu ambaye anadondosha simu yake mara kwa mara, anashauriwa kununua kava ambalo ni kubwa kidogo ili kuilinda simu yake. Kwa mtu ambaye simu yake hutulia mfukoni na haidondoshi, anaweza kununua kava jembamba ambalo linaendana na muundo wa simu yake.

Mbembwe

Kava za simu zinakuja na mbembwe nyingi hivyo cha kuzingatia ni kama mbwembe iliyopo kwenye kava yako itakurahisishia matumizi ya simu yako.

Mfano, zipo kava ambazo zina kipete cha kushikilia simu yako wakati  unatazama filamu.

Pia zipo kava ambazo zimeunganishwa na betri kwa ajili ya kuchaji simu. Unaweza kuziita kava za “power bank” hizi zitamfaa mtu ambaye anatumia simu kwa muda mrefu hivyo kuhitaji chaji ya ziada.

Mahitaji na eneo la kazi

Unaponunua kava lako hakikisha unazingatia mahitaji yako pamoja na eneo la kazi. Mfano, tovuti ya wire imeainisha kuwa zipo kava kwa ajili ya kuitumia simu yako hata ndani ya maji na zipo ambazo zinaziba sehemu ambazo maji hayatakiwi kuingia.

Kwa ambao wanaishi kwenye mazingira ya vumbi, zipo pia kava ambazo zinazuia vumbi kuingia kwenye simu yako na kuzuia madhara kwenye kifaa hicho.

Hali yako ya usafi

Unawezaje kwenda kununua kava jeupe wakati unaijua hali yako ya usafi inahitaji maombi?

Pale unapochagua kava, hakikisha unachagua la rangi ambayo inaendana na usafi wako au hali halisi ya matumizi.

error: Content is protected !!