CCM yapanga kuongeza mchango wa sekta ya utalii kwenye Pato la Taifa

HomeKitaifa

CCM yapanga kuongeza mchango wa sekta ya utalii kwenye Pato la Taifa

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinataka mchango wa sekta ya utalii ufike asilimia 20 katika Pato la Taifa ifikapo mwaka 2030.

Katika Ilani ya Uchaguzi wa Mwaka 2025-2030 CCM imeeleza sekta ya utalii ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya taifa kwa ujumla na itaielekeza serikali iongeze wigo wa mazao ya utalii na kuendelea kuitangaza hazina ya utalii kwa mbinu za kisasa.

CCM imeeleza itafanya hivyo ili mchango wa sekta ya utalii katika Pato la Taifa kutoka asilimia 17 mwaka 2025 hadi asilimia 20 mwaka 2030.

Chama hicho tawala kimesema kitaielekeza serikali iimarishe mikakati ya kutangaza na kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi kwa kuanzisha kampeni maalumu ya kufikisha idadi ya watalii 8,000,000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2030.

Aidha, CCM itaelekeza serikali iongeze ajira kwenye sekta ya utalii kutoka ajira milioni 1.5 mwaka jana hadi ajira milioni tatu ifikapo mwaka 2030 kwa kuongeza uwekezaji katika maeneo ya utalii na ujuzi katika fani za utalii ukiwamo uongozaji wa watalii, huduma kwa wateja na usimamizi wa hoteli.

 

error: Content is protected !!