MSD yapokea bilioni 100 kwa ajili ya kuongeza uzalishaji

HomeKitaifa

MSD yapokea bilioni 100 kwa ajili ya kuongeza uzalishaji

Bohari ya Dawa (MSD), imepokea zaidi ya shilingi bilioni 100 ikiwa ni mtaji wa kuimarisha uwezo wake wa kifedha kwa kuongeza uzalishaji wa dawa na upatikanaji wa wake nchini.

Hayo yalibainishwa Bungeni Dodoma jana na Naibu Waizri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, alipojibu swali la Boniphance Getere (Bunda-CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua kwanini tangu mwaka 2018 hadi hivi sasa MSD haijapeleka majokofu manne ya mochwari katika kituo hicho.

Akijibu swali hilo, Dk. Mollel alisema jokofu hilo lilifikishwa katika kituo hicho Februari 21, mwaka jana na linaendelea kufanya kazi vizuri.

“Serikali itaendelea kununua na kusambaza vifaatiba katika vituo vya kutolea huduma za afya kulingana na upatikanaji wa fedha,” alisema.

Pia, Dk. Mollel alisema serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 980 za kuboresha na kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bunda, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wakazi wa wilaya hiyo.

error: Content is protected !!