Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amekabidhi jengo la kupumzikia wananchi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambalo litasaidia kutatua changamoto ya wananchi wengi ambao hawakuwa na eneo lenye staha la kupumzika wakati wakiwa wanawahudumia wagonjwa wao.
Hafla hiyo ya kukabidhi jengo hilo iliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary S. Senyamule.
“Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan amefanya kazi kubwa ya maboresho ya vifaa na huduma ya Afya kwenye Hospitali hii ya Rufaa Dodoma.
Kazi iliyofanywa na Mbunge Mavunde ni ya kuigwa mfano kwa kuwa ameunga mkono jitihada za Mh. Rais kwenye maboresho ya huduma za Afya.
Jengo hili litasaidia sana kuwafanya wananchi wa Dodoma na nje ya Dodoma kukaa kwenye mazingira mazuri na nadhifu,hivyo naagiza jengo hili kutunzwa na kusimamiwa vyema kwa lengo lililokusudiwa.
Nakupongeza pia Mbunge Mavunde kwa kuanzisha ujenzi wa uzio wa Hospital ya Rufaa,nitoe rai kwa wadau wengine kuunga mkono jitihada hizi kubwa za Mbunge katika kuweka uzio wa Hospitali ya Rufaa”Alisema Senyamule