CCM yazindua Harambee ya kuchagia fedha kwa ajili ya kampeni

HomeSiasa

CCM yazindua Harambee ya kuchagia fedha kwa ajili ya kampeni

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua rasmi harambee ya kitaifa kwa lengo la kuchangia fedha za kufanikisha kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza Agosti 11, 2025 katika ofisi ndogo za CCM Makao Makuu, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema maandalizi hayo yanahitaji nguvu kubwa ya kifedha, ikiwemo ununuzi au ukodishaji wa magari, uchapishaji wa vipeperushi, mabango, tisheti, kanga, mafuta na gharama nyinginezo.

Ameeleza kuwa hatua hiyo imechochewa na hamasa ya wanachama wa CCM, ambao hadi sasa wamefikia zaidi ya milioni 13.19 waliosajiliwa kidijitali, na sasa wanashirikishwa katika uchangiaji.

Harambee hiyo itafanyika Agosti 12, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City kuanzia saa 11 jioni, ikihudhuriwa na wanachama na wadau wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo fedha zitakazopatikana zitatumika kuimarisha mikakati ya ushindi wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu.

error: Content is protected !!