Vituo 50 vya kuhifadhia parachichi kujengwa nchini

HomeKitaifa

Vituo 50 vya kuhifadhia parachichi kujengwa nchini

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Mbeya kuwa Serikali imejikita katika kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi, kwa kuwekeza katika mazingira bora ya kazi na biashara.

Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya katika muendelezo wa mkutano wa Kampeni za Urais uliofanyika leo Septemba 5, 2025 katika viwanja vya Tandale.

Katika hotuba yake,Dkt. Samia amebainisha kuwa moja ya maeneo ya kipaumbele ni sekta ya kilimo, hususan uzalishaji wa parachichi, ambao sasa umepata soko la kimataifa.

Vilevile, ameongeza kuwa Serikali imepanga kujenga vituo 50 vya kuhifadhi parachichi nchini, ambavyo vitakuwa na miundombinu ya baridi ili kuongeza muda wa uhifadhi wa zao hilo.

Akifafanua zaidi, Dkt. Samia amesema miongoni mwa vituo hivyo, viwili vitajengwa wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.

Mgombea wetu Rais Dkt. Samia ameyasema haya ;

“Vituo hivi vitahifadhi parachichi kwa muda wa hadi miezi mitatu ili tukisubiri mataifa mengine yakamilishe msimu wao wa uzalishaji na sisi tuweze kuuza parachichi zetu kwa bei nzuri sokoni”

Aidha, Kuhusu zao la chai, Dkt. Samia ameeleza kuwa Serikali itaunda timu maalumu kwa ajili ya kufanya tathmini ya mashamba na viwanda vya chai, ambavyo vimekabidhiwa kwa kampuni binafsi lakini hazijatekeleza majukumu yao ipasavyo.

error: Content is protected !!