Nuh Mziwanda afunguka haya juu ya Shilole

HomeBurudani

Nuh Mziwanda afunguka haya juu ya Shilole

Mwanamuziki wa bongofleva Nuh Mziwanda, amefunguka na kueleza kuwa bado ana mpenda msanii na mfanyabiashara Zuwena maarufuku kama Shilole na kusema kuwa anajua Shilole bado anampenda na kwa upande wake yuko tayari kurudiana naye kwani bado ana nafasi ndani ya moyo wake.

Nuh amesema kwamba chanzo cha kutofuta tattoo ya Shilole ni kwamba bado anampenda na anaamini ipo siku watarudiana na kuendeleza mahusiano yao kama zamani.

“Mapenzi ya kweli hayafi mzee alafu mimi binadamu nina uhuru wa kuongea, kama nitakuwa namkera mtu sawa lakini bado yupo ndani ya moyo wangu,” 

Nuh Mziwanda afuta tattoo ya Shilole

“Mimi naamini katika wanaume wote duniani mimi ndio mwanaume ambaye nampenda kuliko mwanaume yoyote na hatoweza kutokea, na yeye pia mimi ndio mwanaume anayenipenda kuliko mwanaume yeyote,” alisema Nuh Mziwanda.

Aidha, Nuh alisema kwamba licha ya yote aliyowahi kufanyiwa na Shilole lakini amekwisha msamehe na yupo tayari kurudiana naye muda wowote kwani bado anampenda.

error: Content is protected !!