Dkt Samia: Tutaongeza kasi kutekeleza tuliyoahidi

HomeKitaifa

Dkt Samia: Tutaongeza kasi kutekeleza tuliyoahidi

Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba kuhakikisha kunakuwa na kasi ya utekelezaji wa ahadi na Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025/30 ili kazi zote zitimizwe ndani ya muda uliopo na ilivyotarajiwa.

Amesema kama alivyoahidi wakati wa kampeni na kama Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025/30 inavyoagiza, kunahitajika kasi ya utekelezaji wa yaliyopangwa iongezwe ili yatimizwe ndani ya muda mfupi.

Rais Samia ametoa maelekezo hayo leo, Ijumaa Novemba 14, 2025 alipohutubia baada ya uapisho wa Waziri Mkuu, Dk Nchemba Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Hata hivyo, amemweleza kuwa utekelezaji wa kazi hizo unahitaji fedha na kwamba Dk Mwigulu ana uzoefu na anajua zilikokuwa zinapatikana, hivyo atamsaidia Waziri wa Fedha atakayeteuliwa kufanikisha hayo.

“Utekelezaji wa kazi zote hizo zinahitaji fedha na wewe umetoka katika sekta ya fedha, kwa muda wa miaka mitano umejua vichochoro vyote tulivyokuwa tukipita kutafuta fedha.

“Kwa hiyo utamsimamia atakayekaa kwenye nafasi yako (Wizara ya Fedha), ili naye aweze kupita kule tulikopita fedha ipatikane na kazi ifanyike. Kwa kifupi una kazi kubwa sana,” amesema.

error: Content is protected !!